Pambazuka

Giza ni jingi kabla ya kucha

Na hata sasa kutapambazuka

Mambo haya ni kwa muda

Janga hili litapita

Kutapambazuka, pambazuka

Pambazuka aaah

Kenya tutainuka, tutainuka

Tutainuka na kunawiri

Tumwamini Mungu, ye huwa hashindwi

Kwa pamoja tutapata ushindi

Tusimame wima, daima sisi Wakenya

Nyota yetu tena, itang’aa

Kutapambazuka, pambazuka

Pambazuka aaah

Kenya tutainuka, tutainuka

Tutainuka na kunawiri

Twajivunia tu wakenya

Nchi nzuri, nchi sawa

Ni dhahiri tu pamoja

Twaungana kwa furaha

Tupambane kwa kila janga

Kutapambazuka, pambazuka

Pambazuka aaah

Kenya tutainuka, tutainuka

Tutainuka na kunawiri

Yale yote yamepita

Mazuri na mabaya

Kwa huzuni na furaha

Bado tunashinda

Tunalo tumaini

Mambo yatakuwa sawa

Nguvu yetu ni umoja

Kutapambazuka

Kutapambazuka, pambazuka

Pambazuka aaah

Kenya tutainuka, tutainuka

Tutainuka na kunawiri

Tushikane, tujaliane

Tusaidiane, tutashinda

Tushikane, tujaliane

Tusaidiane, tutashinda

Kutapambazuka, pambazuka

Pambazuka aaah

Kenya tutainuka, tutainuka

Tutainuka na kunawiri

Kutapambazuka, pambazuka

Pambazuka aaah

Kenya tutainuka, tutainuka

Tutainuka na kunawiri

Pambazuka Video

Search for song or artist
New Lyrics
Submit Lyrics

Would you like to contribute lyrics? Please submit them here.

Browse artists